Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk chini ya udhibiti wa Ukraine kuhama kutokana na kuongezeka kwa mapigano.
Eneo hilo limeshuhudia mapigano makali huku kukiwa na mwendo wa polepole wa vikosi vya Urusi kusonga mbele, ambavyo tayari vinadhibiti sehemu yake kubwa.
"Tutatumia fursa zote zinazopatikana kuokoa maisha ya watu wengi iwezekanavyo na kupunguza ugaidi unaotekelezwa na Urusi kadiri iwezekanavyo".
Kuingilia kati kwa Zelensky kunakuja wakati Urusi imewaalika maafisa wa Umoja wa Mataifa na Msalaba Mwekundu kuchunguza vifo vya wafungwa 50 wa vita wa Ukraine katika sehemu nyingine ya mkoa Donetsk.
Wakizungumza Jumamosi jioni, maafisa wa ulinzi wa Urusi walisema Moscow itakaribisha uchunguzi wenye "malengo’’ kuhusu tukio hilo na pia ilichapisha orodha ya kile ilichosema ni wafungwa wa kivita 50 waliouawa katika shambulio hilo.
#ChanzoBBC