Kaimu rais wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe ametangaza sheria ya hali ya hatari
Katika juhudi za kutuliza vurugu za umma na kuushughulikia uchumi ulioporomoka wa taifa hilo la kisiwa. Tangazo lililotolewa na serikali yake limesema ni sahihi kuchukua hatua kama hiyo kwa maslahi ya usalama wa watu, na kuhakikisha usambazaji wa mahitaji muhimu kwa jamii. Rais wa Sri Lanka aliyetimuliwa madarakani, Gotabaya Rajapaksa ambaye wiki iliyopita aliikimbia nchi, amesema alifanya kila awezalo kuepusha kusambaratika kwa uchumi wa taifa lake. Wickremesinghe ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Rajapaksa ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kuwania rasmi wadhifa wa rais, ingawa waandamanaji waliomfukuza mtangulizi wake wanataka yeye pia afungashe virago na kuondoka.
CHANZO: DW SWAHILI