Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema hawawezi kumruhusu Putin kushinda vita.
Scholz ametoa kauli hiyo wakati akitoa hotuba ya nusu saa yenye maswali na majibu mafupi katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos.
Amelaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, lakini hajataja ukosoaji unaotolewa dhidi ya serikali yake kwa kuchelewa kuiunga mkono Ukraine kwa msaada ambao Rais Volodymyr Zelensky aliuomba juu ya kupatiwa silaha.
"Hatuwezi kumruhusu Putin kushinda vita hivi," anasema, na kuongeza "hakutakuwa na amani iliyoamriwa".
Katika hotuba yake, amesema Ujerumani inakamilisha kile kinachojulikana kama "Zeitenwende" au hatua ya kubadilisha sera ya kigeni, kwa kusambaza silaha kwenye eneo la vita kwa mara ya kwanza.
#ChanzoBBC