Star Tv

Maafisa wa jeshi wa Ukraine wanasema wamefanikiwa kuziangusha ndege kadhaa za kijeshi za Urusi katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Maafisa hao wanataja ndege nne, helkopta 3 na zingine ndogo ambazo hazijatajwa zinazoonekana kuwa ni za jeshi la Urusi.

Ukraine inasema imeanza kufanya mashambulizi ya anga kwenye vituo vya kijeshi na maghala ya vifaa vya kijeshi vya Urusi, ili kuvuruga mifumo yake ya ysambazi silaha kwenye mpaka wa Ukraine.

Imeongeza kwamba vikosi vya Urusi havijaweza kusonga mbele, vikijielekeza zaidi kujiimarisha kaika maeneo ambayo tayari imesambaza majeshi yake.

Taarifa hiyo ya Ukraine inasema miundo mbinu ya kiaraia ikiwemo maeneo ya kuabudu yamekuwa yakiangaziwa na majeshi ya Urusi na kupeleka huko Silaha na vifaa vingine vya kijeshi.

Mpaka sasa BBC haijaweza kuthibitisha madai haya ya Ukraine.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.