Star Tv

Mtu mmoja amefunguliwa mashtaka ya mauaji baada ya kudaiwa kuukata mguu wa mtu mwingine huko kaskazini-mashariki mwa Australia.

Mwanaume mwenye umri wa miaka 66, alifariki katika bustani ya Innisfail, Kaskazini mwa Queensland, mapema Jumamosi baada ya kukutwa na wapita njia, polisi walisema.

Polisi wanaamini kuwa mwanaume huyo na mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 36 walikuwa na mpango fulani ambapo kijana huyo alimkata mguu mzee.

Polisi wamesema kuwa wanaume hao wawili wanaonekana kufahamiana, polisi, Aidha wamebainisha kuwa watu hao waliendesha gari hadi kwenye bustani hiyo pamoja kisha dakika 20 baadaye, mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 36 anadaiwa kumkata mguu mwingine chini ya goti.

Kisha mshukiwa alimsaidia majeruhi huyo kurudi kwenye gari kabla ya kuondoka eneo hilo kwa miguu.

Mpita njia alimpata mtu aliyejeruhiwa na kupiga simu za dharura, lakini mzee huyo wa miaka 66 alipoteza maisha muda mfupi baadaye.

"Katika kipindi cha miaka 34 kama afisa wa polisi, sijawahi kukumbana na hali kama tunavyowasilishiwa hapa leo," - Inspekta wa Upelelezi Gary Hunter aliviambia vyombo vya habari vya Australia.

Inspekta wa Upelelezi Gary Hunter ameviambia vyombo vya habari vya Australia kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na kusema kuwa haijafahamika ni kwa nini mguu wa mwanaume huyo ulikatwa.

#ChanzoBBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.