Waziri mkuu wa Libya Abdulhamid al-Dbeibah, amesema leo kuwa anazingatia mpango wa kusuluhisha mzozo wa kisiasa nchini humo na huenda akatangaza mpango wa serikali katika siku zijazo.
Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al Ahrar, Dhbeiba amesema lengo la mpango wake litakuwa kuandika rasimu ya sheria ya uchaguzi kwa ajili ya bunge la nchi hiyo.
Pia ametangaza utayari wake kujiondoa katika kinyang'anyiro cha urais ili kuwezesha kufanikiwa kwa mpango huo.
Awali al-Dbeibah, alisema hatua ya bunge kuichagua serikali mpya ni jaribio jingine la kuingia Tripoli kwa nguvu, huku Umoja wa Mataifa ukisema utaendelea kumuunga mkono, licha ya bunge kumchagua Fathi Bashagha kuchukua nafasi yake.
#ChanzoDW