Star Tv

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikataa kufanyiwa vipimo vya Covid nchini Urusi kabla ya mkutano wake na Rais Vladimir Putin wa Urusi, Kremlin imethibitisha.

Uchunguzi huo ulihitaji itifaki ya afya ambayo haikubaliki na haiendani na ratiba ya kiongozi huyo wa Ufaransa, chanzo cha Ufaransa kiliambia BBC.

Hatua hiyo inafuatia ripoti kwamba Macron alikataa kipimo cha PCR kwa hofu kwamba Warusi wangepata DNA yake.

Viongozi hao baadaye walifanya mkutano huku wakiwa wamekaa mbali kijamii siku ya Jumatatu.

Hawakusaliamia kwa mikono na kukaa na meza yenye urefu wa mita nne kati yao, huku waangalizi wakishangaa iwapo Putin alikuwa akiitumia njia hiyo kutuma ujumbe wa kidiplomasia.

Lakini vyanzo vya kidiplomasia vya Ufaransa viliiambia Reuters kwamba Bw Macron alikuwa ameambiwa achague kati ya kukubali vipimo vya PCR vya Urusi ili kuwa karibu na Putin au kutii sheria kali za kukaa mbalimbali.

Tulijua vizuri kwamba hatua hiyo ilimaanisha kwamba hakutakuwa na kusalimiana kwa mkono katika meza hiyo ndefu. Lakini hatukubali waweze kupata DNA ya rais, moja ya vyanzo hivyo aliambia Reuters.

Chanzo hicho hakikuelezea jinsi huduma hiyo ya ujasusi wa Urusi ingetumia DNA ya bwana Macron.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema kwamba Urusi inaelewa uamuzi huo wa Ufaransa na haikuathiri mazungumzo.

#ChanzoBBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.