Mashambulizi ya mtandaoni ya Korea Kaskazini yameiba mamilioni ya dola za sarafu ya digitali ili kufadhili programu za makombora nchini humo, ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyoarifu vyombo vya habari inasema.
Kati ya 2020 na katikati ya 2021 wavamizi wa mtandao waliiba zaidi ya dola milioni 50 (£37m) ya mali ya kidigitali, wachunguzi walibaini.
Mashambulizi kama haya ni "chanzo muhimu cha mapato" kwa programu ya nyuklia na makombora ya balestiki ya Pyongyang, walisema.
Matokeo hayo yaliripotiwa kukabidhiwa kwa kamati ya vikwazo ya Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa.
Mashambulizi hayo ya mtandaoni yalilenga takribani ubadilishanaji wa awamu tatu wa sarafu za kimtandao huko Amerika Kaskazini, Ulaya na Asia.
Ripoti hiyo pia ilirejelea utafiti uliochapishwa mwezi uliopita na kampuni ya usalama ya Chainalysis ambayo ilisema mashambulizi ya mtandaoni ya Korea Kaskazini yangeweza kuingiza mali ya kidigitali zenye thamani ya dola milioni 400 mwaka jana.
Mnamo mwaka 2019, UN iliripoti kwamba Korea Kaskazini ilikuwa imekusanya takribani dola bilioni mbili kwa programu zake za maangamizi makubwa kwa kutumia mashambulio ya kisasa ya mtandao.
Korea Kaskazini imepigwa marufuku na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanya majaribio ya nyuklia na kurusha makombora ya balistiki.
Hata hivyo ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema licha ya vikwazo ilivyowekewa, Korea Kaskazini imeweza kuendelea kutengeneza miundombinu yake ya nyuklia na makombora ya balestiki.
#ChanzoBBC