Star Tv

Jeshi nchini Burkina Fasso linasema kwamba limechukua mamlaka na kumuondoa madarakani rais Roch Kabore.

Tangazo hilo lilitolewa katika runinga ya taifa na afisa mmoja wa jeshi, ambaye alisema kwamba aserikali na bunge limevunjwa.

Kufikia sasa haijulikani bwana Kabore yuko wapi, lakini afisa huyo amesema kwamba wale wote wanaozuiliwa wapo katika eneo salama.

Mapinduzi hayo yanajiri siku moja tu baada ya wanajeshi hao kudhibiti kambi za jeshi huku milio ya risasi ikisika katika mji mkuu wa Ouagadougou.

Mapema, Chama tawala cha peoples Movement PMP kilisema kwamba wote Kabore na waziri mmoja wa serikali walinusurika jaribio la mauaji.

Siku ya Jumapili, wanajeshi waasi walitaka kufutwa kazi kwa maafisa wa jeshi na kuongezwa kwa raslimali za kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu.

Taarifa hiyo ilitolewa na kundi ambalo halijasikika hapo awali, Vuguvugu la Patriotic for Safeguard and Restoration au MPSR, kifupi chake cha Kifaransa.

"MPSR, ambayo inajumuisha vitengo vyote vya jeshi, imeamua kusitisha wadhifa wa Rais Kabore leo,"-Ilisema Taarifa hiyo.

Kabla ya tangazo hilo, Muungano wa Afrika na Umoja wa Afrika Magharibi Ecowas walilaani kile walichokiita jaribio la mapinduzi nchini Burkina Faso.

ECOWAS imesema kwamba wanajeshi watawajibikia usalama usalama wa Bw Kaboré iwapo lolote litatokea.

Huduma za mtandao wa simu za mkononi zimekatizwa, ingawa mtandao wa laini zisizobadilika na wi-fi ya nyumbani zinafanya kazi

Bw Kaboré hajaonekana hadharani tangu mzozo huo uanze lakini machapisho mawili yalionekana kwenye akaunti yake ya Twitter kabla ya afisa huyo kutangaza kuwa amepinduliwa.

Siku ya Jumapili, mamia ya watu walijitokeza kuwaunga mkono wanajeshi hao na baadhi yao walichoma moto makao makuu ya chama tawala. Amri ya kutotoka nje wakati wa usiku imewekwa.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.