Star Tv

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo umesema kuwa unaafiki ushirikia wa kikanda wa kukabiliana na risho linalovuka mipaka la waasi hao.

Kauli hii inakuja baada ya majeshi ya DRC na Uganda kuanzisha operesheni ya pamoja ya "kuwawinda" wapiganaji kutoka kikundi cha Allied Democratic Forces (ADF) baada ya kushutumiwa kufanya mashambulio ya kujitoa muhanga katika mji mkuu wa Uganda Kampala, mwezi uliopita.

Majeshi hayo mawili yanafanya operesheni za anga na ardhini dhidi ya waasi wa ADF.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa nchini Congo, Mathias Gillman, aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Kinshasa Jumatano kuwa hatua hiyo ni “chaguo halali kisheria na uamuzi wa mamlaka za Wacongo”.

“Tunazishauri nchi za kanda kushirikiana kutatua tisho linalovuka mpaka. Congo ilichukua uamuzi huo kupambana na ADF, na tunauheshimu," Bwana Gillman aliongeza.

Umoja wa Mataifa umekuwa na kikosi kikubwa cha wanajeshi wake mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa miongo miwili iliyopita.

Lakini mapema mwaka huu, maandamano yalitikisa miji ya Goma na Beni ambapo watu walitoa wito wa kumalizika kwa operesheni za Umoja wa mataifa, wakisema kuwa umoja huo umedhihirisha "kukosa ufanisi" ikatika juhudi za kupata utulivu nchini humo.

Tarehe 6 Disemba Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepanga kuamua iwapo kikosi chake kitaendelea kuwepo DRC au laah.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.