Star Tv

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa Ethiopia iko katika hatari ya kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Umoja wa Mataifa umesema wafanyakazi wake 16 wamezuiwa katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema wengine sita wameachiliwa huru.

Alisema Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imetakiwa kuwaachilia wote mara moja.

Bado haijabainika kwanini walikamatwa. Mwezi uliopita maafisa saba wakuu wa Umoja wa Mataifa walifukuzwa baada ya kushutumiwa kuingilia masuala ya Ethiopia.

Umoja wa Mataifa umezungumza kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na umeishutumu serikali kwa kuzuia utoaji wa misaada kwa mamilioni ya waathirika wa mgogoro kaskazini mwa Ethiopia.

Kumekuwa na shutuma nyingi kwamba watu wa Tigray wamekamatwa kiholela jambo ambalo serikali inakanusha.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.