Star Tv

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Malala Yousafzai "amefunga pingu za maisha" na mpenzi wake wakati wa sherehe za Kiislamu huko Birmingham.

Mwanaharakati huyo mwenye umri wa miaka 24 alisema ilikuwa "siku ya thamani" katika maisha yake.

Yeye na Asser Malik walishiriki katika sherehe ya nikkah, ambapo bibi na bwana harusi wanaruhusiwa kuoana.

Mwanaharakati huyo wa haki za wanawake wa Pakistan alipata hifadhi Magharibi mwa Midlands baada ya kupigwa risasi kichwani na Taliban mwaka 2012.

"Mimi na Asser tumefunga pingu za maisha kuwa wenzi wa maisha," aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumanne, akielezea jinsi walivyoshiriki katika sherehe ndogo ya nikkah na familia.

Malala, ambaye sasa ana umri wa miaka 24, alikuwa na umri wa miaka 15 alipolengwa risasi na Taliban nchini Pakistan alipozungumza kutetea haki ya wasichana kupata elimu.

Alinusurika katika shambulio hilo, ambapo mwanamgambo alipanda basi lake la shule kaskazini-magharibi mwa bonde la Swat na kufyatua risasi, na kuwajeruhi marafiki zake wawili wa shule pamoja na yeye mwenyewe Malala.

Baada ya kupona majeraha, yeye na familia yake walihamia Birmingham, ambako baadae alikuita nyumbani kwake kwa pili.

Katika umri wa miaka 17, alikuwa kijana mdogo kupata ushindi wa tuzo ya amani ya Nobel. Alienda kusoma chuo kikuu cha Oxford, na kuwa kinara wa kampeni za kutetea haki za binadamu.

#ChanzoBBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.