Taliban imepiga marufuku matumizi ya fedha za kigeni nchini Afghanistan, hatua ambayo inaelezwa kwamba itaathiri zaidi uchumi wao ambao unaporomoka.
Taliban inafikia hatua hiyo mara baada ya hali ya kiuchumi bado haijatengamaa kutokana na kujiondoa kwa msaada wa kifedha wa kimataifa mara baada ya Taliban kuingia madarakani.
"Hali ya ya uchumi na matakwa ya taifa katika nchi yanahitaji raia wote wa Afghans kutumia fedha za Afghani katika biashara zao,"- Taliban ilisema.
Dola ya Marekani ilikuwa ikitumka zaidi katika masoko ya Afghanistan.
Dola pia zimekuwa zikitumika mara nyingi katika biashara za maeneo ya mpakani mwa Afghanistan kama Pakistan.
"Yeyote atakayekiuka sheria hii atakabiliwa na hatua za kisheria,"- taarifa Kutoka nchini humo zimeeleza.
Baada ya Taliban kudhibiti taifa hilo mwezi Agosti, mabilioni ya dola yaliyokuwa nje ya nchi yalitaifishwa na Marekani.
#ChanzoBBCSwahili