Star Tv

Viatu vya aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya kikapu nchini Marekani Michael Jordanvimeuzwa kwa bei ya $1.47m (£1.1m) iliovunja rekodi katika mnada.

Jordan alitumia viatu hivyo aina ya Nike Air Ships vyenye rangi nyekundu na nyeupe wakati wa msimu wake wa kwanza akiichezea timu ya Chicago Bulls.

Huo ndio mwaka yeye na Nike walianza ushirikiano wao kuunda nguo zenye nembo yake na viatu. Bei hiyo ndio ya juu zaidi kwa viatu vya michezo.

Jordan anaaminika na wengi kuwa mchezaji bora zaidi katika historia ya mchezo wa vikapu.Jordan ambaye kipindi kirefu aliichezea timu ya Chicago Bulls alikuwa nyota na kuweza kuinua kiwango cha mchezo huo kote duniani.

Jordan ambaye alistaafu mwaka 2003 alikuwa mchezaji wa kwanza Bilionea katika historia ya NBA.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.