Star Tv

Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Kanali Mamady Doumbouya anatarajiwa kuapishwa leo kama rais wa mpito.

Sherehe ya kuapishwa kwake itafanyika katika ikulu ya rais na itahudhuriwa na wale walioalikwa pekee.

Kanali Doumbouya aliongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais Alpha Condé mapema mwezi uliopita.

Anatarajiwa kuunda serikali katika wiki chache zijazo.

Kiongozi huyo wa kijeshi aliye na miaka 41, atakuwa kiongozi wa pili wa Afrika mwenye umri mdogo kuongonza nchi, mdogo zaidi akiwa ni wa Mali Kanali Assimi Goïta, 38 ambaye aliongoza mapinduzi ya kumng’oa madarakani Rais Keïta.

Baada ya mapinduzi ya Guinea Kanali Doumbouya alisema askari wake wamechukua uongozi na walitaka kumaliza ufisadi, ukiukwaji wa haki za binadamu na usimamizi mbaya uliokithiri nchini humo.

Rais Condé alichaguliwa katika uchaguzi uliokumbwa na utata kuongoza kwa muhula wa tatu licha ya maandamano ya ghasia mwaka jana.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.