Star Tv

Rais wa Tunisia amemfukuza kazi Waziri Mkuu pamoja na kusitisha shughuli za bunge, kufuatia kuzuka kwa vurugu za maandamano katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana na kupambana na Polisi siku ya Jumapili ili kuonyesha hasira zao dhidi ya serikali kwa namna inavyolishughulikia vibaya suala la Covid-19.

Rais Kais Saied alitangaza kusimamia suala hilo kwa kusaidiwa na waziri mkuu mpya, akisema anataka kuleta utulivu nchini humo. Lakini wapinzani wake wanasema hatua aliyoichukua Rais huyo ni kama mapinduzi ya kimamlaka.

"Tumechukua hatua hizi... mpaka hali ya Tunisia irejee kuwa shwari, mpaka tukiokoe nchi,"-Alisema Saied katika hotuba yake kwenye televisheni baada ya kuitisha kikao cha dharura cha usalama.

Usiku wa Jumapili, waandamamaji walilipuka kwa shangwe kufuatia taarifa kwamba waziri mkuu Hichem Mechichi amefukuzwa kazi na Rais wake.

Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana mjini Tunis na majiji mengine dhidi ya chama tawala wakipaza sauti zao kwa kusema "ondokeni!", na kutoa wito wa bunge kuvunjwa.

Vikosi vya Usalama vilizuia maeneo ya Bunge na mitaa kadhaa karibu na eneo la Avenue Bourguiba, lililokuwa kitovu cha maandamano makubwa ya mwaka 2011 dhidi ya serikali yaliyoleta mapunduzi makubwa nchini Tunisia.

Polisi walipiga mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji hao na kuwakamata watu kadhaa, huku mapambano yakizuka baina yao katika miji kadhaa.

Waandamanaji hao walivamia ofisi za chama tawala cha Ennahdha party, kuharibu Kompyuta,pamoja na kuchoma moto kwenye ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho huko Touzeur.
#ChanzoBBCSwahili

Latest News

KENYA YAPIGA MARUFUKU FILAMU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA.
23 Sep 2021 14:44 - Grace Melleor

Bodi ya Filamu Kenya inasema kuwa filamu kuhusu maisha ya wanandoa wa jinsia nchini Kenya imepigwa marufuku nchini humo. [ ... ]

SHIL. MIL. 700 ZATOLEWA KUKARABATI BARABARA KARAGWE.
23 Sep 2021 13:55 - Grace Melleor

Serikali imetoa Shilingi Milioni 700 kusaidia ukarabati wa barabara za vijijini katika jimbo la Karagwe mkoani Kagera il [ ... ]

BABA AKAMATWA KWA KUCHOMA 'MATITI' YA BINTI YAKE.
22 Sep 2021 13:32 - Grace Melleor

Polisi katika jimbo la Nigeria la Lagos wamemtia nguvuni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwen [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.