Idadi ya watu waliofariki kutokana na mfululizo wa milipuko katika kambi ya jeshi katika Jamhuri ya Guinea ya Ikweta imeongezeka na kufikia watu 98.
Maafisa wa wa Wizara ya Afya wanasema mlipuko huo ulitokana na silaha ambazo zilihifadhiwa vibaya ambayo ilichomeka baada ya moto uliowashwa na wakulima katika shamba lililokuwa karibu.
Idadi ya waliofariki iliongezeka baada ya wadumu wa kujitolea kuchukua karibi siku nzima kutafuta miili katika vifusi. Awali ilikadiriwa ni watu 31 pekee ndio waliofariki kutokana na mkasa huo.
Wizara hiyo imesema kuwa majeruhi 299 bado wako hospitalini wanaendelea kupata matibabu, Huku kundi la wataalamu wa afya ya kiakili pamoja na wauguzi wanaendelea kuwahudimia waathiriwa wa mkasa huo.
Karibu majengo yote na nyumba za makazi katika mji huo ziliharibiwa vibaya na mlipuko huo, Rais Teodoro Obiang Nguema alisema.
Katika taarifa, Rais Obiang Nguema alisema mlipuko huo ulisababishwa na uzembe uliohusishwa na hifadhi ya baruti kali katika kambi ya kijeshi ya Nkoantoma.