Star Tv

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka siku ya Jumatatu, umesafirishwa kwenda mjini Roma.

Luca Attanasio, mlizi wake Vittorio Lacovacci, na dereva wake raia wa DR Congo Moustapha Milambo, waliuawa katika shambulio lililofanywa dhidi ya msafara wa magari ya chakula ya Umoja wa Mataifa, Mashariki mwa nchi hiyo.

Ndege ya kijeshi ya Italia iliyokuwa imebeba majeneza mawili yaliyokuwa yamefunikwa bendera ya kitaifa ilitua katika uwanja wa ndege wa Ciampino mjini Roma na kupokelewa na Waziri Mkuu, Mario Draghi.

Mamlaka nchini DR Congo zimelaumu kundi la waasi wa Rwanda la FDLR kwa mauaji, Lakini pia kundi hilo limekanusha kuhusika na shambulio hilo.

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.