Star Tv

Rais wa Marekani Joe Biden amesema hatua ya Baraza la Seneti ya kumuondolea mashtaka rais wa zamani Donald Trump ya kuchochea vurugu kwenye majengo ya bunge ni jambo linalokumbusha kuwa demokrasia imedhoofika.

Biden ameyasema hayo saa chache baada ya Baraza la Seneti kushindwa kupata theluthi mbili ya kura ili kumtia hatiani Trump, anayekuwa kiongozi wa kwanza wa Marekani kushtakiwa mara mbili mbele ya Bunge.

Bwana Biden amesema mwenendo huo unaonesha jinsi demokrasia inavyochechemea na kuwatolea wito raia wa nchi hiyo kusimama kidete kulinda ukweli na kupinga aina zote za hadaa.

Katika kura ya jana maseneta 57 ikiwemo 7 kutoka chama cha Trump cha Republican, walipiga kura ya kumtia hatiani rais huyo wa zamani huku 43 wakikataa mashtaka dhidi yake.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.