Star Tv

China imekataa kutoa data muhimu kwa timu ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) inayochunguza asili ya Covid-19, mmoja wa wanachama wake alisema ni utaratibu wa kawaida.

Dkt Dominic Dwyer aliyaambia mashirika la habari ya Reuters, Wall St Journal na New York Times timu hiyo iliomba data ya mgonjwa mpya kutoka kwa wagonjwa wa awali, kile alichokiita "mazoezi ya kawaida" na kuambulia kupokea muhtasari tu.

China haijajibu madai hayo lakini hapo awali imesisitiza ilikuwa wazi kwa WHO.

Marekani imeitaka China kutoa data zinazopatikana kutoka katika hatua za mwanzo za mlipuko ikisema ina "wasiwasi mkubwa" kuhusu ripoti ya WHO.

Wiki iliyopita, timu ya WHO ilihitimisha kwamba "haiwezekani kabisa" kwamba virusi vya corona vilivuja kutoka kwenye maabara katika jiji la Wuhan, ikiondoa nadharia yenye utata iliyoibuka mwaka jana.

Wuhan ilikuwa mahali pa kwanza ulimwenguni ambapo virusi hivyo viligunduliwa, mwishoni mwa 2019. Tangu wakati huo, zaidi ya watu milioni 106 walipata maambukizi na vifo vya watu milioni 2.3 vimeripotiwa ulimwenguni.

Wachunguzi walikuwa wanaomba data za watu 174 waliombukizwa Covid-19 kutoka Wuhan mwezi Desemba 2019, Profesa Dwyer aliiambia Reuters.

Ni nusu tu ya watu waliokuwa wameambukizwa awali vilikuwa kwenye soko la vyakula vya baharini ambapo virusi hapo awali viligunduliwa.

Thea Kolsen Fischer, mtaalam wa kinga wa Denmark ambaye pia alikuwa sehemu ya timu ya WHO, aliiambia New York Times kwamba aliona uchunguzi huo ni "wa kisiasa sana".

"Kila mtu anajua kuna shinikizo kiasi gani kwa China kuwa wazi kwa uchunguzi na pia ni lawama ngapi zinaweza kuhusishwa na hii," alisema.

Prof. Dwyer alisema vizuizi vya kupata data vitatajwa katika ripoti ya mwisho ya timu ya WHO, ambayo inaweza kutolewa mapema wiki ijayo.

Timu hiyo iliwasili mapema Januari na ikakaa wiki nne nchini China - mbili za kwanza katika karantini hotelini.

Chanzo na BBC Swahili.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.