Star Tv

Rais wa Marekani Joe Biden ametumia mazungumzo yake ya kwanza na mwezake wa China Xi Jinping kuelezea wasiwasi wa Washington juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye jimbo la Xinjiang na tabia ya mabavu inayotumiwa na China katika shughuli za uchumi.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani imesema katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jana, Biden pia amezungumzia ukandamizaji unaofanywa na China kwenye mji wa Hong Kong na mwenendo wa nchi hiyo kwenye kanda ya Asia ikiwemo kuhusu suala la Taiwan.

Kwa upande wake Xi ametumia mazungumzo hayo kumuonya Biden kujiepusha na uhasama ambao amesema unahatarisha ustawi wa nchi hizo mbili na ulimwengu kwa jumla.

Kulingana na shirika la habari la China, Xinhua, rais Xi amemtaka Biden kuheshimu maslahi ya Beijing ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari anaposhughulikia masuala ya Hong Kong, Taiwan na Xinjiang akisema hayo ni mambo ya ndani ya China.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.