Star Tv


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amemchagua mwanamke wa kwanza kuwa Katibu katika Baraza la mkutano wa Maaskofu.

Nathaniel Becquart, ambaye anatoka Ufaransa atakuwa na haki za kupiga kura katika baraza hilo ambalo hutoa ushauri kwa Papa na kushiriki katika mijadala inayohusisha masuala tata katika kanisa hilo.

Bi Becquart amefanya kazi katika baraza la mikutano hiyo kama mshauri tangu 2019.

Katibu mkuu wa bodi hiyo, Kadinali Mario Grech, alisema kwamba uteuzi huo umeonesha kwamba 'mlango umefunguliwa'.

Amesema kwamba uamuzi huo unaonesha lengo la Papa la kutaka wanawake wengi zaidi kushiriki mchakato wa utambuzi na maamuzi katika kanisa hilo.

Mwandishi wa BBC John McManus anasema kwamba hatua hiyo sio sababu ya kuwafanya wanawake kuwa makuhani, japokuwa wanaopinga wanasema kwamba ni hatua inayoelekea upande huo.

Luis Marin de San Martin, ambaye ni Kuhani kutoka Uhispania pia aliteuliwa kuwa Katibu katika Baraza hilo linalompatia ushauri Papa.

Katika miaka ya hivi karibuni Sinodi ya Maaskofu imejadili mada za mafundisho ikiwemo jinsi ya kuwachukulia Wakatoliki waliotalakiana mbali na wale walioolewa.

Habari hii inakuja chini ya mwezi mmoja baada ya Papa Francis kubadilisha sheria katika Kanisa kuwaruhusu wanawake kuhudumu katika madhabahu ingawa amri hiyo ilisisitiza kwamba ukuhani utabaki wazi kwa wanaume pekee.

Mwaka jana, wakati huohuo, Papa Francis aliwateua wanawake sita kwenye baraza linalosimamia fedha za Vatican.

Chanzo na BBC Swahili.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.