Star Tv

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi kusaidia kufanyika kwa mazungumzo nchini Belarus na kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa.

Kiongozi wa upinzani nchini Belarus Svetlana Tsikhanouskaya baada ya mkutano na rais wa Ufaransa nchini Lithuania amewaambia waandishi wa habari kuwa;

"Ametuahidi kufanya atachoweza kusaidia kufanyika kwa mazungumzo katika mgogoro wa kisiasa ambao nchi yetu unapitia....itabidi mchakato huo wende haraka kwa sababu watu wengi wanateseka kwa kutokana na utawala, watu wengi wako gerezani, na atafanya kila awezalo kusaidia kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa".

Kiongozi wa Upinzani Svetlana Tsikhanouskaya alitoroka nchi yake baada ya uchaguzi wa Agosti 9 ambao Rais anayemaliza muda wake Alexander Lukashenko alitangazwa mshindi, hali ambayo imesababisha maandamano makubwa nchini humo, maandamano yanayoendelea kuzimwa kwa nguvu za kupita kiasia na mamlaka.

Emmanuel Macron anafanya ziara yake ya kwanza Lithuania na Latvia tangu Jumatatu wiki hii hadi Jumatano, nchi mbili za Baltic ambazo ana imani kuwa zitasaidia katika mgogoro huo wa kisiasa nchini Belarus na shinikizo la Urusi.

Umoja wa Ulaya na nchi za Baltic hazijatambua uchaguzi wa Lukashenko na Lithuania inaendelea kumpa hifadhi ya ukimbizi kiongozi wa upinzani nchini Belarus Svetlana Tikhanovskaïa.

Belarus haikuwahi kuwa nchi ya pekee hadi karne ya 20 na maeneo yake yalikuwa chini ya himaya mbalimbali kama vile Poland, Lithuania na Urusi. Belarus ilikuwa kitengo cha Umoja wa Kisoviet tangu 1919/1922 hadi 1991.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.