Saudi Arabia imetangaza kwamba mkutano wa nchi zilizostawi kiviwanda na kiuchumi (G20) utafanyika kwa njia ya video tarehe 21 na 22 Novemba mwaka huu.
Katika taarifa yake, Saudi Arabia, imesema mkutano huo utakuwa na kauli mbiu ya "Kuzipa uhalisia fursa za karne ya 21 kwa ajili ya wote".
Mkutano huo utakuwa kwa njia ya mtandao badala ya kukutana mjini Riyadh kama ilivyokuwa imepangwa mwanzoni
Kundi hilo la mataifa 20 linakusanya theluthi mbili ya idadi ya watu ulimwenguni, likiwa na asilimia 85 za uchumi na 75 ya biashara.
Mkutano wa kilele wa G20 huwaleta pamoja viongozi kutoka mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea ulimwenguni kuzungumzia ustawi wa maendeleo ya viwanda.