Star Tv

Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta amejiuzulu muda mfupi baada ya kuwekwa kizuizini na Jeshi la nchi hiyo.

Akilihutubia taifa lake kwa njia ya televisheni,Keïta amesema anaivunja serikali na bunge akisema ''Sitaki damu imwagike ili mimi kuendelea kubaki madarakani''.

Hatua hii imekuja saa kadhaa baada ya kiongozi huyo wa juu na Waziri Mkuu Boubou Cissé kupelekwa kwenye kambi ya jeshi karibu na mji mkuu Bamako, hatua iliyosababisha mataifa ya Afrika Magharibi na Ufaransa kulaani kitendo hicho.

''Ikiwa leo, sehemu ya vikosi vilivyo na silaha wanataka hili liishe kwa kuingilia kati, nina cha kufanya?'' alisema Keïta.

Rais huyo pamoja na waziri mkuu wake walikamwatwa na jeshi baada ya maandamano yaliyodumu kwa miezi kadhaa kumtaka bwana Keita kung'atuka madarakani.

Keita ambaye alikua katika muhula wake wa pili wa uongozi alikua akituhumiwa kusababisha mdororo wa kiuchumi nchini humo pamoja na kushindwa kuyazuia makundi ya wapiganaji wa kiislamu ambayo yameharibu amani ya nchi hiyo.

Yaya Sangaré ambaye ni msemaji wa serikali amesema Rais Ibrahim Boubakar Keita na waziri mkuu Boubou Cisse wapo katika mikono ya jeshi la nchi hiyo.

Hii inatajwa kwamba ni muendelezo wa kile kilichoanza kama maandamano ambayo yamedumu kwa miezi kadhaa sasa kupinga utawala wa Keita anayeshutumiwa kuisababishia nchi mdororo wa kiuchumi.

Maandamano yamedumu kwa miezi kadhaa sasa huku wachambuzi wa masuala ya siasa tayari wamelitaja tukio hili kuwa ni la mapinduzi.

Kukamatwa kwake kumewafurahisha maelfu ya waandamanaji ambao wamekua mitaani kila uchao kupinga utawala wake.

Katika maandamano mengine makubwa ya mwaka 2012, wapiganaji wa kiislam walilichukua eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo huku kukiendelea kuwa na ukosefu wa amani na kushuhudiwa mapigano baina ya jeshi na vikosi vya wapiganaji wa kiislam katika maeneo kadhaa nchini humo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.