Star Tv

Umoja wa Afrika umetishia kuisimamisha Sudan kufuatia mapinduzi ya wiki iliyopita yaliyoshuhudia Omar al-Bashir akiondolewa madarakani na jeshi. Katika taarifa yake Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, limesema ikiwa jeshi litashindwa kukabidhi madaraka kwa raia ndani ya siku 15, basi Umoja wa Afrika utasitisha ushiriki wa Sudan katika shughuli zote za Umoja huo hadi pale amri ya kikatiba itakaporejeshwa.

Bashir ameitawala Sudan kwa miaka 30 kabla hajaondolewa wiki iliyopita kufuatia maandamano ya nchi nzima yaliyoanza mwezi Desemba. Hata hivyo Umoja huo umesifu madai ya waandamanaji na kuita uingiliaji wa jeshi kuwa ni mapinduzi ambayo umeyalaani. Umoja wa Afrika ulio na wanachama 55 umeongeza kuwa serikali ya mpito ya kijeshi itakuwa ni tofauti matakwa ya watu wa Sudan. Umoja huo umekuwa na msimamo mkali kuhusiana na mapinduzi na uliwahi kuzisimamisha Misri na Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2013 kufuatia mapinduzi katika nchi hizo mbili.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili ya DW

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.