Baraza la kijeshi linaloongoza nchini Sudan limesema leo kwamba baraza hilo limeapa kwamba serikali mpya itakuwa ya kiraia.
Mkuu wa kamati ya kisiasa ya baraza la mpito la jeshi hilo, Omar Zeinalabdin, amesema baraza hilo halitalazimisha kitu chochote kwa wananchi, na linataka kutengeneza hali ya mjadala wa amani. Amesema katika mkutano na waandishi habari leo kwamba baraza hilo lina mpango wa kuanza mjadala na makundi ya kisiasa baadaye leo. Baraza la mpito la kijeshi linatarajia kipindi cha mpito kilichotangzwa jana kuwa kwa kipindi cha miaka miwili, na kusema kipindi hicho kinaweza kufupishwa hadi mwezi mmoja iwapo kitaendeshwa bila mparaganyiko.
CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI YA DW