Star Tv

Mgombeaji urais atakayepeperusha bendera ya chama cha Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Joseph Kabila katika uchaguzi mkuu nchini humo Desemba atatangazwa leo Jumatano kwa mujibu wa msemaji wa rais. Wanachama wa muungano unaojulikana kama Common Front for Congo (FCC) waliitwa kwenda kasri la rais nje ya mji wa Kinshasa jana Jumanne kwa kile kilitajwa kuwa "mkutano muhimu.

Baada ya mazungumzo hayo ya mapema jana, msemaji wa Kabila Lambert Mende, aliwaambia waanidishi wa habara kuwa mngombea atajulikana mapema asubuhi. Wakati wa mkutano wa Jumanne kwenye shamba lake, Rais Kabila aliwatubia wale waliofika bila ya kutaja hatma yake ya kisiaisa.

Kabila ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 alikataa kuandoka mwishoni mwa mwaka 2016 wakati mihula yake miwili ya kikatiba ilikamilika lakini bado amekataa kusema ikiwa atawania tena. Baadhi ya wapinzani wake wanashuku kuwa kabila atajaribu kubaki madarakani na kuwania kwa muhula wa tatu licha ya katiba kutoruhusu hilo.

Sintofahamu hiyo imechangia kuzuka misukosuko ya kisiasa na kusababisha maandamano ya kumpinga kabila ambayo yamesababisha umwagikaji wa damu. Baadhi ya watu ambao huenda wakapendekezwa na Kabila ni pamoja na waziri mkuu wa zamani Augustin Matata Ponyo; Mkuu wa watumishi wa rais, Nehemie Mwilanya Wilondja; na rais wa bunge la taifa Aubin Minaku.

Nchi ya Jamhuri wa Demokrasia ya Congo yenye karibu watu milioni 80 haijakuwa na mabadiliko amani ya madaraka tangu ipate uhuru wake mwaka 1960.Kabila ambaye sasa na miaka 47 alichukua madaraka kutoka kwa baba yake Laurent-Desire Kabila, ambaye aliuawa na mlinzi wake. Muda wake uongozi umekumbwa na ufisadi, kutokuwepo usawa na ghasia.

Shirika la Transparency International liliiorodhesha DRC nambari 156 kati 176 nchi fisadi zaidi duniani mwaka 2016. Mikoa mingi inakumbwa na mizozo na mamilioni ya watu wamekimbia makwao wengine wakielekea nchini Uganda, Tanzania, Angola na Zambia.

Wagombea ambao tayari wametangaza kuwa watawania urais ni Jean-Pierre Bemba, 55, mbabe wa zamani wa vita na hasimu wake Kabila ambaye alirejea Kinshasa wiki iliyopita baada ya kuondolewa mashtaka ya uhalifu wa kivita na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya huko Hague.

Mgombea mwingine wa upinzani Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), naye aliwasilisha makaratasi yake siku ya Jumanne. Mgombea mwingine ambaye alitangaza kuwani Jumanne ni Tryphon Kin-Kiey Mulumba aliyekuwa wakati mmoja msemaji wa Mobutu Sese Seko na ambaye alihudumu mara mbili kama waziri wa serikali ya Kabila ambaya ni mgombea huru.

Mwishoni mwa wiki iliyopita mamlaka zilimzuia Moise Katumbi, 53, mfanyabiashara tajiri na gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga kuwasilisha makaratasi yake ya kuwania urais. Katumbi amekuwa akiishi nchini Ubelgiji tangu Mei mwaka 2016 baada ya kutofautiana na Kabila.

Kwa Hisani Ya BBC Swahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.