Star Tv

Wapiga kura Zimbabwe wanaelekea debeni katika uchaguzi wa kwanza pasi kuwepo kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe miongoni mwa wagombea. Kiongozi huyo muanzilishi, Mugabe alitimuliwa katika mapinduzi mwaka jana baada ya kuwa madarakani kwa takriban miongo minne.

Wagombea wakuu katika uchaguzi wa urais ni kiongozi aliyepo Emmerson Mnangagwa,wa chama tawala Zanu-PF na kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa. Uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa pia zinafanyika leo Jumatatu.

Kura za kutafuta maoni zinampa uongozi mdogo Mnangagwa, mwenye miaka 75, dhidi ya mpinzani wake mwenye miaka 40 anayekiongoza chama cha Movement for Democratic Change (MDC). Hapo jana kiongozi wa zamani Robert Mugabe - aliyeingia kwa mara ya kwanza madarakani mnamo 1980 -

Kunashuhudiwa idadi kubwa ya watu wanaopiga kura kwa mara ya kwanza nchini , ambako kura ya vijana ndio inayotazamwa kuwa na uzito. Takriban nusu ya watu waliosajiliwa kupiga kura wapo chini ya miaka 35. Mamia ya waangalizi wametumwa kuhakikisha uchaguzi unakwenda sambamba, lakini mara kwa mara upinzani umetuhumu kuwepo udanganyifu katika daftari la wapiga kura.

Wameelezea wasiwasi pia kuhusu usalama wa makaratasi ya kupiga kura na kunyanyaswa kwa wapiga kura hususan katika maeneo ya mashinani. Uchaguzi huo unafuata miongo kadhaa ya utawala wa unyanyasaji uliosababisha changamoto kubwa za kiuchumi kwa taifa hilo.

Hili linajumuisha masuala ya uwekezaji, elimu, afya na ajira - takwimu kadhaa zinaashiria kwamba ukosefu wa ajira upo juu kwa 90%. Rais Mnangagwa, anayejulikana kama "Mamba" ameahidi kuhakikisha kuna nafasi za ajira na anaonekana kukubali kuidhinisha mageuzi ya kiuchumi.

Ameponea majaribio kadhaa ya kuuawa ambapo wafuasi wa Mugabe wanatuhumiwa kuyatekeleza. Chamisa, kwa upande wake alikuwa mbunge akiwana umri wa miaka 25, huenda akawa kiongozi mwenye umri mdogo nchini.

Amneahidi kuujenga upya uchumi wa taifa hilio ,lakini ameshutumiwa kwa kutoa ahadi za matumizi ya kupindukia - kama vile kuidhinishwa kwa treni ya mwendo kasi na kuhakikisha mashndani ya kimataifa ya Olimpiki yanaandaliwa Zimbabwe.

Mugabe, aliyejiuzulu mnamo Novemba mwaka jana wakati jeshi lilipochukua udhibiti wa nchi , amekataa kumuunga mkono aliyekuwa mshirika wake Mnangagwa. Kwa kujibu kauli hiyo, Mnangagwa amemtuhumu aliyekuwa kiongozi wake kwa kula njama na upinzani.

"Ni wazi kwa kila mtu kuwa Chamisa amekula njama na Mugabe, hatuwezi tena kuliamini lengo lake la kuigeuza na kulijenga upya taifa letu," amesema. Mugabe pia amekataa pia kwamba alipokuwa rais alipanga kukabidhi uongozi kwa mkewe, Grace, akieleza kuwa uliwa ni "upuuzi mtupu".

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.