Star Tv

Nyota wa zamani wa kandanda duniani George Opong Weah ameapishwa kuwa rais wa Liberia katika sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu Monrovia.

 

Weah amechukua nafasi ya rais wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa kuongoza taifa la Afrika Ellen Johnson Sirleaf, ambaye amestaafu.

Kuingia kwa Weah madarakani kunakamilisha shughuli ya kwanza ya amani ya mpito nchini humo tangu mwaka 1944.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wa mataifa kadha pamoja na nyota wa kandanda duniani.

Akihutubu baada ya kula kiapo, Bw Weah amesema: "Nimekuwa katika viwanja vingi maishani, lakini sijawahi kuhisi hivi."

Bw Weah ameahidi kujitolea kuwatumikia raia wa nchi hiyo. "Nitafanya zaidi ya mchango ninaotarajiwa kutoa ili kutimiza matarajio yenu - lakini naomba nanyi mtimize matarajio yangu, siwezi kutimiza haya peke yangu."

Kiongozi huyo ametumia hotuba yake kusifu uhusiano wa karibu kati ya taifa hilo na Marekani na China.

Kadhalika, amezungumza kuhusu Umoja wa Ulaya. Amesema: "Bila bara Ulaya, Weah hangekuwa amesimama hapa leo."

Weah alicheza mpira wa miguu katika klabu kadha za Ufaransa na Uingereza miaka ya 1980 na 1990 na akaibuka Mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Fifa ya Mchezaji bora wa mwaka duniani na tuzo ya Ballon d'Or.

 Didier Drogba kutoka Ivory Coast ni miongoni mwa wachezaji mashuhuri ambao wamehudhuria sherehe hiyo katika uwanja wa Samuel Doe viungani mwa mji wa Monrovia.

Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa maseneta katika bunge la Liberia.

Aligombea urais mwaka 2005, na alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini akashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki katika duru ya pili.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.