Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhesimiwa Dk.Hussein Ali Mwinyi, awasili jijini Luanda Angola.
Mhesimiwa Dk.Hussein Ali Mwinyi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za kumuapisha Rais wa Jamhuri ya Angola Mhe. Joao Manuel Goncalves Lourenco, pamoja na Makamu wa Rais Esperanca Maria Eduardo Franscisco da Costa. Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Afrika na Nje ya Afrika. Katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Angola Quatro de Fevereiro Mheshimiwa Rais Dk. Mwinyi akiambatana na mkewe Mariam Mwinyi na ujumbe alifuatana nao alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Tete Antonia.