Star Tv

Waandamanaji katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameshambulia na kuharibu kambi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa kushinika ziondoke nchini humo.

Monusco inalaumiwa kwa kushindwa kuleta amani mashariki mwa DRC kwa zaidi ya miaka 20 tangu vikosi hivyo kupelekwa katika eneo hilo linalokumbwa na ghasia.

Picha zilizoshirikishwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakiimba kupinga uwepo wa vikosi vya kulinda amani nchini DRC, wengine wakiondoa nyenzo za msingi wa kituo chao kikuu huko Goma.

Masoko na maduka mengi yamefungwa Jumatatu katika mji unaokaribia watu milioni moja kwa hofu ya kuzuiwa na waandamanaji, Eliezer Makambo mfanyabiashara wa ndani aliiambia BBC Maziwa Makuu.

Msemaji wa serikali, Patrick Muyaya, amesema kwenye Twitter kwamba serikali "inalaani aina yoyote ya mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na majengo".

Muyaya ameongeza kwa kubainisha waliohusika na maandamano ya Jumatatu mjini Goma "wataadhibiwa vikali".

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.