Star Tv

Watoto saba wameuawa nchini Niger katika shambulio la anga la jeshi la Nigeria likiwalenga "majambazi", gavana wa eneo hilo na vyombo vya habari vya serikali vimesema.

Watano wengine walijeruhiwa katika shambulio hilolinaloonekana kuwalilifanywa kwa bahati mbaya, gavana wa eneo la Maradi nchini Niger aliambia AFP.

Gavana Chaibou Aboubacar alisema wanne waliuawa papo hapo na watatu walifariki wakiwa njiani kupelekwa hospitalini. Televisheni ya taifa ilisema shambulio hilo lilitokea katika kijiji cha Nachade.

Bw Aboubacar alisema wazazi wa waathiriwa walikuwa wakihudhuria sherehe na "watoto hao yamkini walikuwa wakicheza" wakati mashambulizi ya anga yalipowakumba.

Aidha amesema anaamini kuwa ndege hizo zilikuwa zikilenga "majambazi wenye silaha" katika maeneo ya mpaka kati ya nchi hizo mbili lakini zilikosa lengo na kugonga kijiji cha Nachade katika eneo la Madarounfa.

Niger na Nigeria zimekuwa zikiendesha operesheni za kijeshi za pamoja dhidi ya magenge yenye silaha yanayohusika na wimbi la utekaji nyara na mauaji katika eneo hilo.

Tangu mwaka 2018 Niger imeimarisha doria za kijeshi katika mpaka wake na Nigeria ili kuzuia uvamizi wa magenge hayo.

Vifo vya watoto hao vimekuja miezi mitatu tu baada ya watoto 26 wenye umri wa miaka mitano na sita kufariki katika ajali ya moto katika shule moja katika mji wa Maradi.

#ChanzoBBC

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.