Star Tv

Umoja wa Afrika umelaani wimbi la mapinduzi ya hivi karibuni ambalo limeshuhudia idadi kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa ya nchi wanachama zikisimamishwa kutoka umoja huo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa baraza la amani na usalama wa Umoja huo Bankole Adeoye wakati kikao cha kila mwaka cha Umoja huo kikikaribia kumalizika.

Adeoye amewaambia wanahabari kwamba kila kiongozi wa Afrika katika baraza hilo amelaani wimbi hilo la mabadiliko ya serikali kinyume na katiba.

Mataifa manne wanachama yalisimamishwa uanchama wao katika Umoja huo tangu katikati ya mwaka 2021 kwasababu ya mabadiliko ya serikali kinyume na katiba.

Mapinduzi ya hivi karibuni zaidi yalitokea nchini Burkina Faso, ambapo wanajeshi walimuondoa madarakani rais Roch Marc Christian Kabore mwezi uliopita.

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.