Star Tv

Wanasayansi nchini Afrika Kusini wametoa nakala yao ya chanjo ya Moderna ya Covid-19, hatua ambayo wanasema inaweza kusaidia kuongeza viwango vya chanjo barani Afrika.

Kwa sasa bara la Afrika lina idadi ndogo zaidi ya watu wanaopata chanjo ya Covid.

Kampuni inayoendesha chanjo hiyo mpya ya Afrigen Biologics inasema inatumai kuanza majaribio ya kimatibabu mnamo mwezi Novemba.

Petro Terblanche, mkurugenzi wa Afrigen Biologics, alisema walikuwa wanaanza kidogo, lakini wana malengo ya kuongeza kasi siku zijazo.

"Tumetumia mpangilio ambao ni sawa na chanjo ya Moderna 1273, Hii ni sehemu ya mpango wa kimataifa wa kujenga uwezo katika nchi za kipato cha chini na cha kati ili kujitegemea" - Petro aliiambia BBC.

Chanjo inayonakiliwa ni ile ya RNA iliyotengenezwa na kampuni ya Kimarekani ya Moderna.

Pfizer-BioNTech pia ilitengeneza chanjo yake kwa kutumia teknolojia hiyohiyo.

Aina hii ya chanjo hufundisha seli jinsi ya kutengeneza protini ambayo itasababisha mwitikio wa kinga ndani ya miili yetu, badala ya kuweka vijidudu dhaifu au visivyotumika mwilini.

Mwanasayansi mkuu wa kampuni hiyo, Dk. Caryn Fenner, alitaja mafanikio hayo " kuwa muhimu sana."

"Inaweka uwezo mikononi mwetu kuweza kutengeneza chanjo zetu wenyewe kwa siku zijazo, kuwa tayari kwa magonjwa zaidi ya milipuko, kutoa nyenzo za majaribio ya kimatibabu katika ardhi ya Afrika na kisha kuangalia magonjwa mengine ya umuhimu barani Afrika."

Nchi nyingi za Afrika zimechanja kikamilifu chini ya asilimia 10 ya watu wake, ikilinganishwa na asilimia 60 Amerika Kaskazini, asilimia 63 Ulaya na asilimia 61 kote Asia.

Licha ya kuwa na viwango bora zaidi barani Afrika, Afrika Kusini imechanja asilimia 27 pekee ya watu wake.

#ChanzoBBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.