Star Tv

Mwanaume mmoja nchini Kenya amekamatwa kwa kosa la kuiba biblia mbili katika duka moja kubwa jijini Nairobi.

Mwanamume huyo ambaye amekamatwa na kushtakiwa kwa kosa hilo amesema alichokuwa akitaka ni kumjua Mungu tu.

Augustine Wanyonyi, 35, ameiambia mahakama kwamba aliiba Biblia hizo ili asome na kumjua Mungu zaidi.

Alipoulizwa kwa nini aliiba nakala mbili badala ya moja, alisema Biblia ya pili alikusudia kwa ajili ya mkewe.

Wanyonyi alifika mbele ya Hakimu Mkuu wa mahakama ya Milimani katika Jiji la Nairobi Susan Shitubi ambapo alikiri kutenda kosa hilo.

"Niliiba biblia ili nisome, nielewe na kuhubiri neno la Mungu badala ya kujiua kutokana na matatizo yanayonikabili," - Wanyonyi aliambia mahakama.

Alishtakiwa mnamo Jumanne tarehe 1 Februari na kurudi mahakamani kuhukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kosa hilo.

Wanyonyi alikamatwa Jumapili baada ya kupatikana na nakala mbili za biblia zenye thamani ya Shilingi 2,100 za Kenya.

Kulingana na ripoti ya polisi iliyosomwa na wakili wa Serikali Alice Mathangani, mshtakiwa alikwenda kwenye duka hilo mwendo wa saa tisa mchana katika tarehe iliyotajwa, na kuiba biblia hizo mbili na kuzificha ndani ya suruali yake.

"Alinaswa na kanda ya CCTV ya duka kuu na baadaye kukamatwa na wahudumu wa CCTV baada ya kushindwa kulipia bidhaa sawa na hiyo alipofika kwa kaunta".Mwendesha mashtaka alisema.

Mwendesha mashtaka pia aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alikuwa na rekodi ya awali ya wizi wa dukani ambapo alishtakiwa Desemba 2021 lakini akaachiliwa na mahakama nyingine baada ya kuomba msamaha.

Hakimu aliamuru ripoti ya kabla ya hukumu iwasilishwe mahakamani ndani ya siku saba. Hivyo atafikishwa mahakamani kuhukumiwa mnamo Februari 16.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.