Kundi la vijana nchini Nigeria, chini ya mwamvuli wa Bunge la Vijana wa Kaskazini, limetoa wito kwa mfanyabishara tajiri zaidi Afrika Aliko Dangote, viongozi wengine wa wafanyabiashara na wataalamu kuingilia kati uchaguzi wa rais wa 2023.
Vijana hao wanasema kuwa uzoefu wao itasaidia kuleta maendeleo Nigeria.Katika taarifa kundi hilo ambalo lilifadhiliwa na Katibu Mkuu wake Desmond Minakaro na Baraza la Wawakilishi, Mohammed Salihu Danlami alisema watu kama Dangote, Femi Otedola, Mike Adenuga, Akinwumi Adesina, Herbert Wigwe, Ngozi Okonjo Iweala na kadhalika wana uwezo wa kuchukua nafasi ya rais wa Nigeria.
Vijana hao wametoa ushawishi wao kwamba “wafanyabiashara wanaojua jinsi ya kupata faida sasa wanapaswa kuitawala Nigeria”.
Hata hivyo seneta Shehu Sani amesema haoni haja ya Bw. Dangote kuingilia siasa na kwamba anamtaka aendelee kuwa maarufu kutokana na utajiri wake mbali na siasa.