Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki zake wamethibitisha juu ya kifo chake.
Miaka miwili iliyopita aliugua kiharusi lakini chanzo cha kifo chake siku ya Jumapili hakikuweka wazi.
Alifariki mwendo wa saa tatu saa za Uingereza nyumbani kwake mjini Bamako, mmoja wa ndugu yake aliiambia chombo cha Habari cha AFP.
Bwana Keita aliiongoza Mali kwa miaka saba hadi 2020, wakati alipopinduliwa kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali kutokana na jinsi alivyolishughulikia suala la Wanajihad.
Mgogoro wa kiuchumi na uchaguzi ulio huru pia ulisababisha maandamano hayo dhidi ya utawala wake.
Bwana Keita alihusika katika siasa kwa zaidi ya miongo mitatu, akihudumu kama waziri mkuu kutoka 1994 hadi 2000.
#ChanzoBBC