Star Tv

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, televisheni ya taifa imeripoti.

Watu takriban 17 wamejeruhiwa, wakiwemo watoto 13 kutoka shule jirani na eneo la tukio.

Mlipuaji mabomu wa kujitoa mhanga wa kikundi cha al-Shabab aliyekuwa anaendesha gari lililosheheni vilipuzi alilenga msafara wa kampuni ya usalama ya kibinafsi, Duguf, ambayo ilipewa kandarasi ya kulinda Umoja wa mataifa.

Polisi haikusema iwapo wafanyakazi wa Umoja wa mataifa waliumia katika shambulio hilo.

Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa mlipuko huo ulitokea wakati wa msongamano wa magari karibu na makutano yanayofahamika kama 'Kilometre Four Junction'.

Kundi lenye uhusiano na Al-Qaeda la wanamgambo wa al-Shabab limethibitisha kutekeleza shambulio hilo.

Vyanzo vya habari vinavyounga mkono al-Shabab media vimesema wanamgambo hao waliwalenga “maafisa wa kijeshi wazungu”.

Mara kwa mara Al-Shabab wamekuwa wakiwalenga maafisa wa vikosi vya usalama na serikali mjini Mogadishu.

#ChanzoBBC

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.