Nyumba ya Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok imezingirwa na wanajeshi.
Vyombo vya habari vinasema kwamba wanajeshi wasiotambulikawameizingira nyumba ya waziri mkuu Abdalla Hamdok.
Runinga ya Al Hadath inaripoti kwamba wanajeshi wamewakamata mawaziri wanne na mwanachama mmoja wa serikali ya mpitokulingana na vyanzo ambavyo havijatambuliwa.
Shirika la Habari la Reuters limeripoti kwamba wanajeshi walivamia nyumba ya mshauri wa masuala ya habari wa waziri mkuu na kumkamata mapema Jumatatu.
Muungano wa Wataalamu nchini humo umewataka raia kuingia barabarani ili kufanya maandamano kwa lengo la kuzuia mapinduzi hayo ya kijeshi.
Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na ripoti kuhusu kuzimwa kwa huduma ya mtandao nchini humo.