Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amewafuta kazi Waziri wa Nishati na mkuu wake wa watumishi ambao wanakabiliwa na mashtaka ya ufisadi.
Wawili hao na afisa mwingine mmoja Enock Chihana, mshirika katika usimamizi wa Tonse Alliance walikamatwa siku ya Jumatatu kwa madai ya kuhusika na zabuni ya mafuta ya nchi hiyo.
Watumishi wa serikali katika wizara nyeti waliripotiwa kujaribu kushawishi jinsi kandarasi ya usambazaji wa mafuta itakavyotolewa.
Nafasi ya waziri Newton Kambala haijajazwa baada ya kufutwa kwake, Ambapo kwasasa majukumu ya wizara ya nishati yamehamishiwa ofisi ya rais.
Mrithi wa mkuu wa watumishi wa umma Chris Chaima Banda pia hajatajwa wakati tangazo la kufutwa kwake lilipotolewa.
Aidha, Bw. Kambala na Bw. Banda hawajatoa tamko lolote kuhusiana na suala hilo.