Watu wenye silaha wamewateka nyara wanafunzi 140 kutoka shule ya sekondari ya Bethel Baptist iliyoko Kaskazini Magharibi mwa Nigeria.
Ripoti hiyo ni kwa mujibu wa afisa wa shule aliyebainisha kwamba watu hao waliivamia shule hiyo na kisha kuwateka wanafunzi 140, ikiwa ni wimbi la karibuni kabisa la utekaji nyara unaowalenga wanafunzi nchini humo.
Watekaji hao walivunja uzio na kuingia katika shule ya sekondari ya Bethel Baptist ambayo ni ya bweni katika jimbo la Kaduna na kuondoka na wanafunzi hao.
Msemaji wa polisi katika jimbo hilo Mohammed Jalinge amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini hakuweza kutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya wanafunzi waliochukuliwa mateka.