Rais wa miaka mingi nchini Zimbabwe anaripotiwa kukataa kuandoka madarakana mara moja licha ya kuongezeka wito wa kumtaka ajiuzulu.
Mugabe, 93 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani wakati jieshi lilichukua madaraka siku ya Jumatano kufuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi.
Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo yaliyofanywa Muganbe na ujumbe kutoka kanda hiyo pamoja na mapema.
Lakini taarifa zinasema kuwa amekataa kuondoka madarakani.
Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai alisema mapema kuwa kwa manufaa ya watu Mugabe anastahili kujiuzulu mara moja.
Jeshi lilichukua hatua baada ya Rais Mugabe kumfuta makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa, wiki iliyopiya, na kuashiria kuwa alimpendelea mke wake Grace Mugabe, kuchukua uongozi wa chama cha Zanu-PF na kuwa rais.
Taarifa zinasema kuwa Mugabe ambaye alikuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwak 1980 anakataa kuondoka kwa hiari kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.