Mfalme Goodwill Zwelithini wa jamii ya Wazulu nchini Afrika Kusini amefariki dunia hospitalini ambako alikuwa anapokea matibabu ya ugonjwa wa kisukari.
Mfalme huyo aliyekuwa na umri wa miaka 72, alikuwa kiongozi wa kabila kubwa zaidi Afrka Kusini na kiongozi mashuhuri wa kitamaduni.
Mfalme huyo alikuwa amelazwa katika hospitali ya Kwa Zulu-Natal wiki iliyopita kufuatilia hali ya kisukari iliyokuwa inamsumbua.
Waziri mkuu wa mfalme huyo ameishukuru Afrika Kusini kwa kuendelea kumuombea na kutoa msaada katika kipindi hiki kigumu.
Mflame Goodwill Zwelithini aliongoza jamii ya Wazulu chini ya kifungu cha sheria ya utawala wa kitamaduni katika Katiba ya Afrika Kusini tangu alipofariki baba yake mwaka 1968.