Star Tv

Serikali ya Ethiopia imeishutumu Sudan kuchochea mgogoro kati ya mataifa mawili ambayo yamekuwa katika mvutano kutokana na mzozo wa mpaka.

Ghasia ziliibuka mwishoni mwa mwaka jana kuhusu eneo la wakulima wa Ethiopia ambao Sudan wanasema waliingia katika eneo lao.

Pande zote mbili zimekuwa zikishutumiana kwa kusababisha ghasia.

Mvutano umekuja wakati Ethiopia ikiwa na mgogoro kaskazini mwa ukanda wa Tigray.

Katika taarifa kali iliyotolewa na serikali ya Ethiopia, imelishutumu jeshi la Sudan kuchochea mvutano huo kuingia kwenye vita.

Licha ya kudai mzozo huu kuhusiana mvutano wa eneo la wafugaji walioko karibu na mpaka lakini inaonekana wazi masuala ya kisiasa kuhusika pia.

Taarifa ya Ethiopia imesema jeshi la Sudan linachochea mgogoro ili kuinufaisha Misri.

Kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya Ethiopia na serikali ya Misri juu ya ujenzi wa bwawa katika mto Nile.

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.