Star Tv

Polisi wamemkamata mwanamume mmoja aliyejulikana kwa jina la Abubakar Amodu mwenye umri wa miaka 20, ambaye alipanga njama na genge moja na kumteka nyara baba yake mzazi na baadaye akapokea milioni 2 za Nigeria kama fidia.

Amodu ni miongoni mwa watu 25 waliokamatwa na afisa wa ofisi ya uhusiano mwema katika polisi ya Nigeria, CP Frank Mba, kwa makosa kadhaa waliotekeleza mjini Abuja.

Kijana huyo aliyekamatwa pamoja na wahalifu wengine, alifaya kazi na baba yake ambaye ni mfugaji.

Kijana huyo aliwaambia wanahabari kuwa baba yake alikuwa anafuga ngombe na kwamba alipewa ngombe 15 na akaamua kuondoka nyumbani.

Alitoa ushahidi vile alivyoanza urafiki na genge hilo la wahalifu waliomshauri kumteka nyara baba yake kwasababu hiyo ilikuwa njia pekee ya kumuwezesha kutengeneza pesa kwa njia rahisi na kutajirika kwa haraka.

Kijana huyo anakiri kwamba, binafsi alipokea milioni mbili pesa taslim za Nigeria kama fidia iliyotumwa ili baba yake aachiwe huru.

Chanzo na BBC Swahili.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.