Star Tv

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amezungumzia vurugu zilizotokea Marekani baada ya wafuasi wa Rais Donald Trump kuvamia jengo la bunge Capitol Hill.

Rais Mnangagwa aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuwa Marekani haina "haki ya kimaadili kuadhibu nchi zingine kwa misingi ya demokrasia".

Alisema kuwa Marekani imeiwekea Zimbabwe "vikwazo vikali" vya kiuchumi.

Mnangagwa amempongeza rais mteule "Ningependa tena kumpongeza Rais mteule Joe Biden, kwa kuthibitishwa kuwa Rais wa 46 wa Marekani, Zimbabwe iko na imekuwa tayari ushirikiano wake kama marafiki na washirika wa Marekani kwa manufaa ya nchi zote mbili," Bwana Mnangagwa amesema.

Marekani na Umoja wa Ulaya zote zimeendeleza vikwazo vyao dhidi ya Zimbambwe kwa madai ya ukosefu wa demokrasia endelevu na mabadiliko ya haki za binadamu pamoja na kubanwa kwa vyombo vya habari.

 

Latest News

RAIS JOE BIDEN AMUONYA RAIS WA URUSI VLADMIR PUTIN
27 Jan 2021 06:39 - Grace Melleor

Rais wa Marekani Joe Biden amemuonya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo.

WANASHERIA WA BOBI WINE WARUHUSIWA KUMUONA MTEJA WAO.
22 Jan 2021 08:40 - Grace Melleor

Jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulany [ ... ]

UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU ABIRIA KUTOKA TANZANIA, DRC.
22 Jan 2021 08:18 - Grace Melleor

Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika matai [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.