Star Tv

Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya amefariki dunia. akiwa na umri wa miaka 71 ,binamu yake na chanzo cha kidiplomasia chathibitishia BBC.

Rais huyo wa Burundi wa zamani amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 71 ,binamu yake na chanzo cha kidiplomasia chaithibitishia BBC.

Chanzo cha familia kimesema alifariki mjini Paris, Ufaransa siku ya Alhamisi kutokana na athari za ugonjwa wa Covid-19.

Jenerali huyo mstaafu alihudumu mara mbili madarakani kwa jumla ya miaka 13 baada ya kuwapindua watangulizi wake madarakani.

Mwezi Oktoba, alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani na mahakama ya Burundi kwa kosa la mauaji ya rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini, Rais Melchior Ndadaye mwaka 1993 ambayo yalisababisha mauaji ya karibu watu 300,000, ambapo alikana kufanya kosa hilo la mauaji.

Mwezi uliopita, alijiuzulu kama mjumbe wa Muungano wa Afrika wa eneo la Sahel, na kusema kuwa anataka kutumia muda wake zaidi kusafisha jina lake.

Marehemu Pierre Buyoya aliingia madarakani kwa mara ya kwanza kama Rais baada ya Mapundizi ya kijeshi dhidi ya utawala wa rais Jean-Baptiste Bagaza mwaka 1987 ambaye pia aliingia madarakani kwa mapinduzi dhidi ya mtangulizi wake Michel Micombero mwaka 1976.

Utawala wake wa miaka sita uligubikwa na mambo mbalimbali ambayo yalibadili sura ya nchi kama vile mauaji ya kinyama yaliyofanyika katika kitongoji cha Ntega-Marangara mwaka 1988, makubaliano ya umoja wa Warundi yaliyoidhinishwa mwaka 1991, kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1993, na mengine mengi.

Aliondoka madarakani mwaka 1993 baada ya kushindwa katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kuwahi kufanyika tangu mwaka 1960. Wakati huo , mtangulizi wake Prezida Melchior Ndadaye kutoka chama cha Frodebu ndiye aliyemshinda kwa asilimia zaidi ya 65% ya kura na Pierre Buyoya aliyekuwa wakati huo amegombea kwa tiketi ya chama cha Uprona aliibuka na 33% za kura.

Buyoya alirejea tena madarakani mwezi wa Julai 1996, baada ya kumpindua tena madarakani rais wa mpito Sylvestre Ntibantunganya, ambaye wakati huo alichukua madarakan kufuatia kifo cha Cyprien Ntaryamira yambaye alikufa katika ajali ya ndege pamoja aliyekuwa rais wa Rwanda wakati huo Juvenal Habyarimana.

Rais Ntaryamira alikuwa ameshikilia kiti cha urais kwa miezi miwili pekee, baada ya kifo cha Rais Ndadaye.

Kuuawa kinyama kwa Rais Ndadaye kulilitumbikiza taifa hilo katika vita vya kikabila , kati ya Watusi na Wahutu nchini humo.

Aidha, Utawala wa rais Buyoya ulitawaliwa na mzozo wa kikakabila baina ya Watutsi na Wahutu.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.