Star Tv

Spika wa bunge la DRC Jeanine Mabunda ameondolewa katika nafasi yake baada ya wabunge kupiga kura ya maoni dhidi yake iliyowasilishwa bungeni na wabunge wa Upinzani.

Miongoni mwa wabunge 484 katika Bunge hilo kura 281 zilisema kwamba kiongozi huyo wa muhimili huyo aondoke katika nafasi yake.

Zaidi ya wabunge 200 kati ya wabunge 500 walifanya kikao cha kupiga kura ya kumuondoa madarakani Spika wa bunge Jeanine Mabunda kutoka chama cha Joseph kabila.

Mwandishi wa BBC, nchini DRC amesema ; Upande wa chama cha Kabila tayari kulikuwa na mzozo katika vyama vilivyokuwa vinamuunga mkono, hivyo hiyo inaweza kuwa sababu ya kuanguka kwao.

Na hatua inayofuata ni Waziri Mkuu kujiuzulu sasa kwasababu rais atamchagua mtu atakayeunganisha vyama bungeni hivyo nia ya rais kuvunja muungano huo.

Aidha, Tuhuma zimemwendea rais wa zamani Joseph Kabila kwa kumchagua mtu dhaifu ambaye hajawahi kuwa kiongozi au kusimamia watu wowote.

Hata kutoka kwa wafuasi wake Kabila wanaona kuwa nafasi ile ilihitaji mtu ambaye ana uzoefu wa kisiasa, tofauti na spika aliyeondolewa.

Huku wabunge wa upande wa rais aliyeko madarakani Felix Tschisekedi wanamtuhumu kwa uongozi mbaya.

Kwa mujibu wa mbunge Moindo Nzangu ambaye aliwasilisha mapendekezo ya kura hiyo mwanzilishi Spika Bi Jeanine Mabunda atatakiwa kujitetea mbele ya wabunge kabla ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Vurugu na ghasia zilitokea ndani ya bunge hilo wiki hii wakati ulipowasilishwa muswada wa kura ya maoni na watu kadhaa walijeruhiwa wakati wanaharakati na wabunge walipoanza kurushiana viti na kuharibu samani ndani ya bunge.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.