Star Tv

Mapigano yametokea kati ya kundi la wanamgambo wa Maï-Maï na vikosi vya jeshi la serikali, FARDC, katikati mwa mji mkuu wa Katanga, ya zamani Kusini Mashariki mwa DRC.

Mapigano hayo yametokea usiku wa Ijumaa kuamkia leo Septemba 26,2020, Ambapo milio ya risasi na milipuko imeendelea kusikika mapema leo Jumamosi aljafajiri karibu na Chuo Kikuu.

Wanamgambo hao waliingia katika mji wa Lubumbashi usiku wakipitia maeneo kadhaa ya mji huo.

Vyanzo vya polisi kupitia Waziri wa Mambo ya Nje Philibert Kunda Milundu amesema wamethibitisha tukio hilo katika mkoa huo na vinahakikisha kuwa wapiganaji hao ni kutoka kundi la wanamgambo la Bakata Katanga, lililojitenga kutoka kundi la Maï-Maï.

Waziri Milundu amesema wanajeshi wamegizwa kutowapiga risasi wanamgambo hao, Huku hali ya wasiwasi pia inaripotiwa katika mji wa Likasi.

Mapigano hayo yanatokea baada ya jaribio la wafungwa kutoroka kutibuliwa siku ya Ijumaa katika gereza la Kasapa huko Lubumbashi.

Chanzo: rfi Swahili.

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.